Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, Majilio ni kipindi cha imani na matumaini yenye furaha. Huu ni mwaliko kwa waamini kumwomba Kristo Yesu katika hija hii kuelekea katika Maadhimisho ya Sherehe ya Noeli, yaani kuzaliwa kwa Kristo Yesu, aweze kuandaa mioyo yao, ili hatimaye, waweze kuwa ni mashuhuda na vyombo vya amani yake. Waamini wanahamasishwa kukesha huku wakisali na kuomba; wakitafakari Neno la Mungu; wakipokea Sakramenti za Kanisa