Liturujia ya Neno la Mungu ya Dominika hii inatualika, “Kuwa macho, kukesha na kuomba” kwa sababu hatujui siku wala saa atakapokuja tena Bwana wetu Yesu Kristo. Katika kipindi hiki cha Majilio, tumwombe Mungu atujalie neema ya kujiandaa vyema kumpokea Kristo, si katika sherehe ya Noeli pekee, bali pia katika maisha yetu ya kila siku. Waamini wanaalikwa kukesha katika Sala, Tafakari ya kina ya Neno la Mungu, katika Sakramenti za Kanisa na Matendo ya huruma.