Parokia, ni mahali ambapo maisha ya Kisakramenti yanapewa uzito wa pekee sanjari na ushuhuda wa Injili ya upendo unaomwilishwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili, kama kielelezo cha ushuhuda wa imani tendaji, sehemu muhimu ya uinjilishaji wa Kanisa kwa ajili ya Kanisa linaloinjilisha. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Kipindi cha Majilio Mwaka B wa Kanisa ametia nia ya kutembelea Parokia tano za Jimbo kuu la Roma.