Maaskofu wameonya kuwa hali ya kutokuwa na amani na utulivu; migogoro na ukosefu wa uhakika wa usalama wa chakula vitaendelea kudhoofisha utu na matumaini ya wananchi wa nchi hizo mbili. Katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka kwa kuwataka viongozi wa kisiasa, Jumuiya ya Kimataifa na wananchi katika ujumla wao kutoa kipaumbele katika: ujenzi wa amani, utawala bora, uwajibikaji, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.