Papa Leo XIV mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme wa Ulimwengu, sanjari na Maadhimisho ya Siku ya 41 ya Vijana Duniani amesema “Ushindi wa Kristo Yesu si ushindi wa kidunia, bali ni ushindi wa Mfalme mnyenyekevu anayejitambulisha na wale walio wadogo zaidi miongoni mwetu. Hivyo, ninawaalika vijana wote kuwa na ujasiri wa kuwa wapole na wanyenyekevu kama Kristo. Upendo wake na uwe nguvu yenu.” Papa Leo XIV