Baba Mtakatifu Leo XIV amewashukuru watawa wa ndani kwa maisha na hasa zaidi kwa sala na anamwomba Mwenyezi Mungu ili Jumuiya za Watawa wa Ndani zisikose kamwe msaada zinazohitaji katika maisha na utume wao. Baba Mtakatifu Francisko anasema, watawa ni nguzo ya sala kwa ajili pamoja na Kanisa. Watawa wa ndani wanaendelea kulitajirisha Kanisa la Kristo Yesu kwa matunda ya neema na huruma inayobubujika kutoka kwa Mwenyezi Mungu.