Kwa Walinzi wa Papa kutoka Uswisi, kambi ya Jeshi si mahali pa kuishi tu, bali ni nafasi ya kudumisha na kuishi kulingana na asili ya mtu. Ni mahali ambapo kumbukumbu hupata sauti, ambapo mila huwa hai, na ambapo kukumbuka milima, mabonde, vijiji, na nyuso za wapendwa huvuka mipaka yoyote ya umbali. Huko kambini kijana ingawa yuko mbali na nchi yake anaweza kurejea nyumbani; si tu kupitia kumbukumbu, bali hasa kupitia tunu alizonazo, mafunzo na imani.