Baba Mtakatifu Leo XIV Dominika tarehe 22 Novemba 2026 amehitimisha Maadhimisho ya Siku ya 10 ya Maskini Duniani kwa kula chakula cha mchana pamoja na maskini wapatao 1,300 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Wageni hao mahususi kwa siku hii, walialikwa kupitia Mashirika mbalimbali ya misaada, Parokia, na Vyama vinavyowahudumia maskini na wahitaji Jijini Roma, na walihudumiwa na watu wa kujitolea kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu cha Italia.