Hija hii inalenga kuimarisha azimio la washiriki katika maisha ya familia za Kikristo, uinjilishaji na kulitumikia Kanisa, huku wakipata msukumo kutoka kwa Mitume, watakatifu na mashahidi wa imani, na kutafakari wito na wajibu wao katika kujenga familia na jamii imara zaidi. Ujumbe huo unaongozwa na Padre Charles Kilonzo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Huduma za Kichungaji na Utume wa Waamini Walei, Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya (KCCB): Uinjilisha na Familia!