Baba Mtakatifu Leo XIV amekazia hoja kwamba, “Ustawi, maendeleo na mafao ya wengi” ni kama lengo kuu. Hakika, ikiwa teknolojia na matumizi yake hayatasimamiwa ipasavyo kwa kuzingatia kanuni za maadili na utu wema, hatari kwa wanadamu zitakuwa kubwa mno kama historia ya hivi karibuni inavyotufundisha, na kama inavyooneshwa kwa masikitiko na hali ya kurudi nyuma tunayoiona leo katika nyanja ya ikolojia kamilifu duniani kote. Uchu wa mali na madaraka!