Mama Kanisa anaadhimisha Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu, Siku ya 41 ya Vijana Ulimwenguni. Kauli mbiu ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu katika Sherehe hii inasema, “Jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu” (Yn 16:33). Lengo la sherehe hii ni kuwakumbusha walimwengu kwamba, Yesu anapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza; Hakuna mamlaka iliyo juu ya Kristo na kwamba, Kristo Yesu ni Alfa na Omega, Nyakati zote ni zake, Amina!