Jumuiya ya Kikatoliki ya Shalom imezaliwa katika maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu, ili kunogesha ari, moyo na utamaduni wa sala miongoni mwa vijana wa kizazi kipya. Kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa mintarafu sera na mbinu mkakati wa uinjilishaji mpya unaosimikwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko; kwa kukazia malezi na makuzi ya maisha ya: kiroho na kiutu. Kwa Mwaka 2026 inaadhimisha Miaka 45 ya Utume wake!