Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Katekesi yake amerejea katika Hija ya Sita ya Kitume nchini Uruguay, Argentina na Peru kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 17 Novemba 2026 ambayo kwa hakika imekuwa na mafanikio makubwa, kupita hata matarajio yaliyokuwepo! Katekesi hii imenogeshwa na sehemu ya Maandiko Matakatifu yasemayo: “Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu. Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani..!