Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 tangu FADICA ianzishwe na Jubilei ya Miaka 400 tangu kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, wajumbe wa FADICA, Jumatano tarehe 18 Novemba 2026 wamekutana na kuzungumza na Papa Leo XIV. Kwa FADICA hija hii ni siku za sala, malezi na majiundo makini pamoja na kuendelea kuimarisha udugu wa kibinadamu, mshikamano na umoja na ushirika wa Kanisa pamoja na Baba Mtakatifu.