⛪ World Christian News

전 세계 기독교 뉴스 — 번역 없이 원문 그대로 · 영어 · Español · Português · Français · Deutsch · 日本語 · 한국어 · 中文 · Русский · العربية · Kiswahili …
기사 1,938건 · 활성 소스 75개 · 마지막 수집 9분 전 · 매시각 자동 업데이트
Vatican News (Kiswahili)

Kalenda ya Liturujia Kipindi cha Majilio Mwaka B wa Kanisa

Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, Majilio ni kipindi cha imani na matumaini yenye furaha. Huu ni mwaliko kwa waamini kumwomba Kristo Yesu katika hija hii kuelekea katika Maadhimisho ya Sherehe ya Noeli, yaani kuzaliwa kwa Kristo Yesu, aweze kuandaa mioyo yao, ili hatimaye, waweze kuwa ni mashuhuda na vyombo vya amani yake. Waamini wanahamasishwa kukesha huku wakisali na kuomba; wakitafakari Neno la
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 14시간 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Tunu Msingi za Michezo: Uaminifu, Ujasiri, Ustahimilivu, Nia Njema

Papa Leo XIV akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wasaidizi wa Kanisa wa Michezo, CSI anasema kwamba, katika hotuba ya kukumbukwa na kugusa hisia iliyotolewa kwa wanamichezo mara baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Papa Pius XII, alizungumzia tunu za michezo kuwa ni: uaminifu, ujasiri, ustahimilivu, nia njema, na udugu wa wote” akizielezea kama fadhila za asili zenye uwezo wa kuweka msingi imara kwa
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 14시간 전
Vatican News (Kiswahili)

Tafakari Dominika ya Kwanza ya Majilio Mwaka B: Kesheni, Salini na Kuomba

Liturujia ya Neno la Mungu ya Dominika hii inatualika, “Kuwa macho, kukesha na kuomba” kwa sababu hatujui siku wala saa atakapokuja tena Bwana wetu Yesu Kristo. Katika kipindi hiki cha Majilio, tumwombe Mungu atujalie neema ya kujiandaa vyema kumpokea Kristo, si katika sherehe ya Noeli pekee, bali pia katika maisha yetu ya kila siku. Waamini wanaalikwa kukesha katika Sala, Tafakari ya kina ya Neno
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 15시간 전
Vatican News (Kiswahili)

Tafakari Dominika ya Kwanza ya Majilio Mwaka B: Matumaini Katika Mungu Baba!

Majilio ni kipindi cha kukesha na kusali, ni wakati wa kutoka katika usingizi wa kiroho, ili kuutafakari ufalme wa Mungu. Kwa matumaini tunamkumbuka Yesu Kristo aliyejifanya mtu huku tukitafakari uwepo wake katika maisha yetu. Kama Mungu kweli na Mtu kweli, Kristu anaupa maana uwepo wetu hapa duniani hadhi ya kimungu akituonesha uzuri wa maisha ya Kimungu. “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 16시간 전
Vatican News (Kiswahili)

Tafakari Dominika ya Kwanza ya Majilio Mwaka B: Injili ya Matumaini

Hiki ni kipindi cha maandalizi ya kusherehekea Noeli, kuzaliwa kwake Yesu Kristo, Emanueli, Mungu pamoja nasi. Na ni kipindi cha kujiandaa kumpokea mtoto Yesu kiroho ili ahuishe maisha yetu, tuweze kuishi kwa upendo, umoja, mshikamano na amani. Hivyo majilio ni kipindi cha kungoja kwa matumaini ujio wa Kristo katika maisha yetu. Ni wakati muafaka wa kukesha katika Sala, Neno la Mungu na Sakramenti
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 21시간 전
Vatican News (Kiswahili)

Hotuba ya Papa Leo XIV Kwa Wakuu wa Mashirika Ya Kitawa na Kazi za Kitume: Uongozi

Papa Leo XIV tarehe 26 Novemba 2026 amekutana na wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume zaidi ya 250 na hivyo kuweza kujibu maswali yao sita. Maana ya msemo amani "Isiyo na Silaha na Inayopokonya Silaha” unahusiana kwa karibu na maneneo ya Kristo Yesu Mfufuka “Amani iwe nanyi” Yn 20:19, 21. “Amani ambayo sote tunaitamani ni amani isiyohitaji silaha, na ambayo kwa hakika ina uwezo wa kuondo
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 1일 전
Vatican News (Kiswahili)

Hotuba ya Papa Leo XIV Kwa Wajumbe wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini

Imekuwa ni fursa ya kutafakari hali ya majadiliano ya kidini sehemu mbalimbali duniani, na kutambua jinsi ambavyo jumuiya za Kikristo, pamoja na waamini wa dini nyingine, wanavyoweza kuchangia kwa ufanisi zaidi katika kujenga amani. Katika ulimwengu unaokabiliwa na migogoro, migawanyiko, na mabadiliko ya kiteknolojia hasa katika zama za teknolojia ya Akili Unde Mkutano huu pia umechunguza jinsi ju
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 1일 전
Vatican News (Kiswahili)

Hotuba ya Papa Leo XIV Kwa Wajumbe wa Baraza La Kipapa La Maendeleo Fungamani

Wajumbe wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu kutoka katika nchi mbalimbali, ujuzi na mitazamo tofauti, inayofumbatwa katika huduma, tarehe 26 Novemba 2026 wamekutana na Baba Mtakatifu Leo XIV kuwakumbusha kwamba, Katiba ya Kitume: “Praedicate Evangelium” imewakabidhi jukumu zito: kushirikiana na Khalifa wa Mtakatifu Petro, kupitia kwa Maaskofu, na Makanisa mahalia katika kuragibi
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 1일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV Kipindi cha Majilio Kutembelea Parokia Tano Jimbo Kuu la Roma

Parokia, ni mahali ambapo maisha ya Kisakramenti yanapewa uzito wa pekee sanjari na ushuhuda wa Injili ya upendo unaomwilishwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili, kama kielelezo cha ushuhuda wa imani tendaji, sehemu muhimu ya uinjilishaji wa Kanisa kwa ajili ya Kanisa linaloinjilisha. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Kipindi cha Majilio Mwaka B wa Kanisa ametia nia
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 1일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Tume ya Taalimungu KImataifa: Mapokeo Ya Kitume & Utamadunisho

Tume ya Taalimungu Kimataifa imefanya mabadiliko makubwa na kwa mara ya kwanza wanakutana kwa kuongozwa na kauli mbiu: Mapokeo ya Kitume na Mifumo ya Kitamaduni ya Kueneza imani. Huu ni mchango mkubwa unaotolewa na Tume hii, tangu baada ya Maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na kutambua katika mwanga wa Injili changamoto na fursa mpya zinazoendelea kujitokeza kutokana na mikitadha ya ta
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV Katekesi Kuhusu Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican: Kuhamasisha Amani

GS 77-93: Kuhamasisha amani na kustawisha Jumuiya ya Kimataifa: Maumbile ya amani, kuepuka vita na kuzuia ukatili wa vita; vita kamili; mashindano ya kujipatia silaha; juhudi za Kimataifa ili kuepuka vita; sababu za magomvi na tiba yake; Jumuiya ya Kimataifa na Taasisi zake; Ushirikiano wa Kimataifa katika mambo ya uchumi; Kanuni zenye kufaa; Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu ongezeko la watu; Jukum
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2일 전
Vatican News (Kiswahili)

Tamko la Baraza la Maaskofu Sudan na Sudan ya Kusini: Haki, Amani, Utu Na Heshima!

Maaskofu wameonya kuwa hali ya kutokuwa na amani na utulivu; migogoro na ukosefu wa uhakika wa usalama wa chakula vitaendelea kudhoofisha utu na matumaini ya wananchi wa nchi hizo mbili. Katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka kwa kuwataka viongozi wa kisiasa, Jumuiya ya Kimataifa na wananchi katika ujumla wao kutoa kipaumbele katika: ujenzi wa amani, utawala bora, uwaj
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 3일 전
Vatican News (Kiswahili)

Padre Erasmo Mligo, Gambera wa Seminari Kuu ya Karoli Lwanga, Segerea, Dar es Salaam.

Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, Sehemu ya Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Mapya Maalum, tarehe 16 Oktoba 2026 lilimteuwa Mheshimiwa Padre Erasmo Mligo kutoka Jimbo Katoliki la Njombe kuwa Gambera mpya wa Seminari kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Segerea Jimbo kuu la Dar es Salaam na kusimikwa rasmi tarehe 14 Novemba 2026. Vitendea Kazi: Sheria za Kanisa, Mwongozo wa Malezi ya Kipadre n
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 3일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Vijana ni Matumaini na Jeuri ya Kanisa! Wekezeni Kwa Vijana

Papa Leo XIV mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme wa Ulimwengu, sanjari na Maadhimisho ya Siku ya 41 ya Vijana Duniani amesema “Ushindi wa Kristo Yesu si ushindi wa kidunia, bali ni ushindi wa Mfalme mnyenyekevu anayejitambulisha na wale walio wadogo zaidi miongoni mwetu. Hivyo, ninawaalika vijana wote kuwa na ujasiri wa kuwa wapole na wanyenyekevu kama Kristo. Upe
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 3일 전
Vatican News (Kiswahili)

Sikukuu ya Kutolewa Bikira Maria Hekaluni! Siku ya Watawa wa Ndani

Baba Mtakatifu Leo XIV amewashukuru watawa wa ndani kwa maisha na hasa zaidi kwa sala na anamwomba Mwenyezi Mungu ili Jumuiya za Watawa wa Ndani zisikose kamwe msaada zinazohitaji katika maisha na utume wao. Baba Mtakatifu Francisko anasema, watawa ni nguzo ya sala kwa ajili pamoja na Kanisa. Watawa wa ndani wanaendelea kulitajirisha Kanisa la Kristo Yesu kwa matunda ya neema na huruma inayobubuji
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 4일 전
Vatican News (Kiswahili)

Mfuko wa Ukarabati wa Kambi ya Walinzi wa Papa Kutoka Uswisi

Kwa Walinzi wa Papa kutoka Uswisi, kambi ya Jeshi si mahali pa kuishi tu, bali ni nafasi ya kudumisha na kuishi kulingana na asili ya mtu. Ni mahali ambapo kumbukumbu hupata sauti, ambapo mila huwa hai, na ambapo kukumbuka milima, mabonde, vijiji, na nyuso za wapendwa huvuka mipaka yoyote ya umbali. Huko kambini kijana ingawa yuko mbali na nchi yake anaweza kurejea nyumbani; si tu kupitia kumbukum
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 4일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV Mashindano ya Baiskeli Ni Chombo Cha Uinjilishaji

Baiskeli ni sehemu ya historia na utambulisho wa tamaduni nyingi; ni chombo cha usafiri kinachowawezesha kuboresha afya zao na kwa upande mwingine, ni chombo kinachoweza kusaidia katika kupata uzoefu na mang’amuzi ya maisha kiroho yenye maana zaidi. Watu wengi wanaendelea kuhifadhi kumbukumbu ya mashindano haya kwani mashindano haya yamekita mizizi yake katika utamaduni na mifumo ya kijamii na hiv
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 4일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV Maadhimisho Siku 10 ya Maskini Duniani: Chakula Na Familia ya Maskini

Baba Mtakatifu Leo XIV Dominika tarehe 22 Novemba 2026 amehitimisha Maadhimisho ya Siku ya 10 ya Maskini Duniani kwa kula chakula cha mchana pamoja na maskini wapatao 1,300 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Wageni hao mahususi kwa siku hii, walialikwa kupitia Mashirika mbalimbali ya misaada, Parokia, na Vyama vinavyowahudumia maskini na wahitaji Jijini Roma, na walihudumiwa na watu wa kujit
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 4일 전
Vatican News (Kiswahili)

Wanaume Wakatoliki Kutoka Kenya Wanatembelea Italia na Ufaransa:

Hija hii inalenga kuimarisha azimio la washiriki katika maisha ya familia za Kikristo, uinjilishaji na kulitumikia Kanisa, huku wakipata msukumo kutoka kwa Mitume, watakatifu na mashahidi wa imani, na kutafakari wito na wajibu wao katika kujenga familia na jamii imara zaidi. Ujumbe huo unaongozwa na Padre Charles Kilonzo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Huduma za Kichungaji na Utume wa Waamini Walei, B
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 5일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV Akutana na Kuzungumza na Vijana wa Majimbo ya Lazio, Italia

Imekuwa ni fursa ya pekee kwa vijana kukutana pamoja, kuishi wakati huu kama Kanisa, na kusikiliza maneno ya PapaLeo XIV. Huu umekuwa ni muda wa: Sala, tafakari na shuhuda mbalimbali kutoka kwa: wachumba waliochumbiana, kijana aliyeongoka hivi karibuni na kupokea Sakramenti ya Ubatizo; Msichana mwenye tajiriba ya kimisionari; Kijana anayetafakari wito wa upadre, msichana anayetafakari wito wa mais
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 5일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV Sherehe ya Kristo Mfalme wa Ulimwengu: Haki! Udugu! Uhuru na Utu

Papa Leo XIV anasema, Kristo Yesu katika Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo 25:31-46 anafunua maana halisi ya haki kupitia mazungumzo yake kuhusu watu waadilifu na waovu na kwamba, Kristo Yesu ni kipimo cha haki kwa sababu ndiye chanzo cha wokovu na kwa njia ya mahusiano na mafungamano na mwanadamu anafunua ukweli wake ndani yake mwenyewe, kinyume kabisa na aina zote za ufisadi. Kristo Yesu ni M
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 5일 전
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Kongamano la Nane la Anga Za Juu: Ustawi, Maendeleo na Mafao ya Wengi

Baba Mtakatifu Leo XIV amekazia hoja kwamba, “Ustawi, maendeleo na mafao ya wengi” ni kama lengo kuu. Hakika, ikiwa teknolojia na matumizi yake hayatasimamiwa ipasavyo kwa kuzingatia kanuni za maadili na utu wema, hatari kwa wanadamu zitakuwa kubwa mno kama historia ya hivi karibuni inavyotufundisha, na kama inavyooneshwa kwa masikitiko na hali ya kurudi nyuma tunayoiona leo katika nyanja ya ikolo
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 5일 전
Vatican News (Kiswahili)

Mkutano wa COP31: Kipaumbe Cha Kwanza: Utu, Heshima Na Haki Msingi za Binadamu

Vatican imewataka viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kuweka utu wa binadamu, haki kijamii na mshikamano katika kiini cha hatua za kimataifa za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikionya kuwa kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi kunatishia maisha na riziki za watu walio katika mazingira magumu zaidi. Papa Leo XIV katika ujumbe wake kwa mkutano wa COP30 alikazia ziaidi utu,
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 5일 전
Vatican News (Kiswahili)

Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme wa Ulimwengu! Siku ya 41 ya Vijana! Msiogope!

Baba Mtakatifu Pio XI alipoguswa kuikumbusha dunia na viongozi wake kuwa ufalme wa kweli ni ule unaosimikwa na Kristu nao si wa kisiasa au wa kijeshi wa kidunia unaotumia mabavu na silaha, bali ni ufalme wa haki, amani, upendo, ukweli na wokovu. Kiti cha enzi cha Mfalme huyu ni Msalaba, ambapo Yesu Kristu mwenyewe alijitoa ili awe dhabihu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu. Kanisa pia linaadhimish
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 6일 전
Vatican News (Kiswahili)

Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme & Siku ya 41 ya Vijana Ulimwenguni

Baba Mtakatifu Leo XIV anawaambia kuwa wasiuogope ulimwengu bali wasonge mbele katika kupambana na maisha kwa kuwa Mungu anawajua, anawapenda, na anawasindikiza kila mmoja katika kila hatua ya maisha yake ya kila siku, na Roho Mtakatifu anatia ndani yao hamu ya kupenda na kupendwa, pamoja na tumaini la kudumu, naye anawasukuma kutafuta uhuru na ukweli. Kihitoria Sherehe ya Kristo Mfalme, iliidhini
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 6일 전
Vatican News (Kiswahili)

Sherehe ya Yesu Mfalme wa Ulimwengu; Siku ya 41 ya Vijana Ulimwenguni 22 Novemba 2026

Mama Kanisa anaadhimisha Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu, Siku ya 41 ya Vijana Ulimwenguni. Kauli mbiu ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu katika Sherehe hii inasema, “Jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu” (Yn 16:33). Lengo la sherehe hii ni kuwakumbusha walimwengu kwamba, Yesu anapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza; Hakuna mamlaka iliyo juu ya Kristo na kwamba, Kristo Yesu ni Alfa
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-20
Vatican News (Kiswahili)

Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Siku ya 41 ya Vijana Ulimwenguni: Sherehe ya Kristo Mfalme 2026

Maadhimisho ya Siku ya 41 ya Vijana Ulimwenguni, ngazi ya Kijimbo sanjari na Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu tarehe 22 Novemba 2026 yananogeshwa na kauli mbiu: "Jipeni Moyo! Mimi nimeushinda Ulimwengu: Ujasiri; Ushindi dhidi ya Ulimwengu; Ushindi wa upendo wa kujisadaka; Ujasiri wa unyenyekevu; Kristo Mfufuka anawakirimia waja wake amani, changamoto ni kufungua mioyo yao kwa Kristo Mfuf
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-20
Vatican News (Kiswahili)

Shirika la Kikatoliki la Ustawi na Maendeleo Mashariki ya Kati: CNEWA: Injili ya Upendo

“Kama Shirika kuu la Kiti Kitakatifu nchini Marekani, kwa ajili ya huduma ya shughuli za: kichungaji, kiutu na kibinadamu kwa Makanisa haya, na kama mwanachama mwanzilishi wa Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Mashariki ya Kati, chombo muhimu sana cha mshikamano kati ya jumuiya za Kikristo Amerika Kaskazini na zile zilizoko Mashariki ya Kati. Kupitia shughuli zao, ukaribu wa Kan
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-20
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Jumuiya ya Kikatoliki ya Shalom Miaka 45: Malezi ya Vijana! Amani

Jumuiya ya Kikatoliki ya Shalom imezaliwa katika maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu, ili kunogesha ari, moyo na utamaduni wa sala miongoni mwa vijana wa kizazi kipya. Kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa mintarafu sera na mbinu mkakati wa uinjilishaji mpya unaosimikwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko; kwa kukazia malezi na makuzi ya maisha ya: kiroho na kiutu. Kwa Mwa
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-20
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Jubilei ya Miaka 400 Ya Kutabarukiwa Kanisa Kuu La Mt. Petro Mjini Vatican

Kanisa kuu la Mtakatifu Petro linaadhimisha Jubilei ya Miaka 400 tangu kutabarukiwa kwake kwa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Papa Leo XIV, Jumatano jioni tarehe 18 Novemba 2026. Katika mahubiri yake, Papa Leo XIV anasema “Kutembelea Kanisa hili Takatifu daima huamsha hisia za kina: tunajawa na mshangao, unaotokana na utakatifu wa imani, nguvu ya historia, na uzuri wa sanaa. Hata hivyo, yot
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-19
Vatican News (Kiswahili)

Kenya na Italia Watiliana Saini Mkataba wa Ulinzi Na Usalama

Tarehe 16 Novemba 2026, Kenya na Italia zilifanya mazungumzo yaliyohitimishwa kwa kutiwa saini kwa Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kenya na Serikali ya Italia kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Usalama. Mkataba huo ulitiwa saini na Mheshimiwa Kipchumba Murkomen na Matteo Piantedosi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia. Lengo kuu ni kukabiliana na uhalifu, biashara haramu ya dawa za kulevya
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-19
Vatican News (Kiswahili)

Papa Leo XIV: Caritas Internationalis: Injili ya Huruma, Upendo Na Mshikamano

Caritas inamwilisha katika maisha na utume wake: upole wa Kristo Yesu kwa watu wote. Wanaleta huruma na upendo wa Mungu katika maisha yao watu kupitia msaada wa kiroho na wa kimwili. Zaidi ya hayo, kupitia utume wao pamoja na yale majitoleo ya mamilioni ya watu wanasimama kidete dhidi ya hali kutojali, kwa kujitolea kwao kwa dhati kuheshimu na kulinda: Utu na heshima waliyopewa na Mwenyezi Mungu w
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-19
Vatican News (Kiswahili)

Wimbo rasmi wa Siku ya Vijana Duniani,Seoul 2027 na lugha za Ishara Kimataifa!

Video nne mpya zinazotumia Lugha ya Ishara ya Kikorea na Lugha ya Ishara ya Kimataifa zinaakisi dhamira ya waandaaji ya kuhakikisha kuwa Siku ya Vijana Duniani inapatikana na kufikika kwa vijana wote. Soma yote
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-19
Vatican News (Kiswahili)

UNESCO,Siku ya Falsafa:thamani ya kudumu kwa maendeleo ya fikra!

Katika kuadhimisha Siku ya Falsafa Duniani kila mwaka,ifikapo Alhamisi ya tatu ya mwezi Novemba, UNESCO imewaleta pamoja wanafikra na watunga maamuzi katika Makao Makuu yake,jijini Paris Novemba 19,2026 kwa ajili ya hotuba ya mwanafalsafa Souleymane Bachir Diagne.Je ni nani huyo mwanafalsafa wa Afrika? Soma yote
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-19
Vatican News (Kiswahili)

Ushuhuda wa Wamisionari Kutoka Kenya Wanaoishi na Kufanya Utume Wao Argentina

Kwa Sr. Lucy Muthikwa na Sr. Emma Ganda, wamisionari kutoka nchini Kenya wanaohudumu nchini Argentina, wanasema Hija ya Kitume ya Papa Leo XIV ilikuwa zaidi ya tukio la kihistoria la kukutana na Khalifa wa Mtakatifu Petro. Ilikuwa fursa ya kutafakari miito yao, kugundua upya kiini cha maisha na utume wa kimisionari na kuimarisha dhamira yao ya kutangaza na kushuhudia Injili katika mazingira tofaut
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-18
Vatican News (Kiswahili)

Hija ya Sita ya Kitume ya Papa Leo XIV Amerika ya Kusini: Muhtasari Wake

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Katekesi yake amerejea katika Hija ya Sita ya Kitume nchini Uruguay, Argentina na Peru kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 17 Novemba 2026 ambayo kwa hakika imekuwa na mafanikio makubwa, kupita hata matarajio yaliyokuwepo! Katekesi hii imenogeshwa na sehemu ya Maandiko Matakatifu yasemayo: “Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu. W
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-18
Vatican News (Kiswahili)

Jubilei ya Miaka 50 ya Mfuko wa FADICA, Miaka 400 Kanisa Kuu la Mt. Petro Mjini Vatican

Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 tangu FADICA ianzishwe na Jubilei ya Miaka 400 tangu kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, wajumbe wa FADICA, Jumatano tarehe 18 Novemba 2026 wamekutana na kuzungumza na Papa Leo XIV. Kwa FADICA hija hii ni siku za sala, malezi na majiundo makini pamoja na kuendelea kuimarisha udugu wa kibinadamu, mshikamano na umoja
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-18
Vatican News (Kiswahili)

Uzinduzi wa Siku ya Dominika ya Ikolojia 2026/2027:Mabadiliko Endelevu jijini Roma!

Siku iliyoundwa kwa ajili ya utambuzi wa kupunguza uchafuzi wa mazingira,foleni ya magari na kurejesha nafasi kwa watu,kujumuika na uendelevu,ilifanyika Domenika ya I ya kiikolojia kwa mwaka 2026/2027,jijini Roma,Novemba 15,ikitoa nafasi za ujumuishwaji katika shughuli za kiutamaduni na kuchangamana."Vatican News,ilizungumza na Bi Isabel De Lorenzo wa kikundi cha"San Lorenzo Danze del Mondo:"'Leo
Vatican News (Kiswahili) Kiswahili 아프리카 2026-11-18